VIFUNGU YA JUMLA‌‌‌‌ Zitsanzo za Migwirizano

VIFUNGU YA JUMLA‌‌‌‌. Kifungu 1: Nyaraka za Mkataba Masharti ya Mkataba na fomu ya Malezo ya mahitaji, Viwango na Vipimo ni sehemu muhimu ya nyaraka za Mkataba na zinapaswa kusomwa pamoja na nyaraka nyingine zote zinazounda Mkataba. Kama ikitokea kuna mgogoro, kipaumbele cha nyaraka kitakuwa kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 6 cha Masharti haya ya Mkataba. Kifungu 2: Tafsiri Katika Masharti haya ya Mkataba maneno yafuatayo yatakuwa na maana zilizotolewa kwayo kama ilivyo hapa chini: Mteja Taasisi ya Serikali inayonunua huduma kama zilivyotajwa kwenye mkataba. Mtoa Huduma Mtu au watu au kampuni ambayo kotesheni yao imekubaliwa na mteja. Huduma Huduma itakayotolewa kulingana na mkataba. Kifungu 3: Maelekezo Maelekezo yanayotolewa na Mteja yatakuwa kwa maandishi. Kwa sababu nyingine yoyote ile maelekezo hayo yakatolewa kwa mdomo, Mtoa Huduma atafuata maelekezo hayo. Katika kipindi cha siku 7 maelekezo yaliyotolewa kwa mdomo yanapaswa kuwa yamethibitishwa kwa maandishi.Kifungu 4: LughaMatangazo yote, maelekezo na mawasiliano au warakawowote wa maandishi unaohusu mkataba utaelezwa bayana katika Masharti Maalumu ya Mkataba.Kifungu 5: Sheria inayotumika‌‌‌‌‌‌‌‌Mkataba, maana yake, fasiri yake, na utekelezaji wake vitaongozwa na Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kifungu 6: Nyaraka za Mkataba zenye Kipaumbele Nyaraka kadhaa zinazofanya mkataba zichukuliwe kuwa zinajieleza kikamilifu lakini kama ikitokea hitilafu yoyote ilenyaraka zenye umuhimu wa kwanza zitakuwa zifuatazo: