MALIPO Kifungu 21: Malipo21.1 Malipo ya Awali Zitsanzo za Migwirizano

MALIPO Kifungu 21: Malipo21.1 Malipo ya Awali. Malipo ya awali ya asilimia iliyotajwa kwenye Masharti Maalumu ya Mkataba ya thamani ya mkataba yanaweza kutolewa baada ya kuwasilisha dhamana inayokubalika katika Masharti Maalumu ya Mkataba. Malipo haya ya awali yatakatwa kwa awamu zinazolingana kwa kila bili itakayowasilishwa na Mtoa Huduma, na lazima zilipwe zote. 21.2 Malipo wakati Kazi inaendelea Malipo yatafanywa kwa Mtoa Huduma wakati kazi inaendelea kila mwezi baada ya kuwasilisha ankara kama huduma iliyotolewa inalingana na masharti ya mkataba. Kwa kila ankara kiasi cha fedha kilichotajwa kwenye Masharti Maalum ya Mkataba kitashikiliwa lakini hakitazidi asilimia 10 ya bei ya mkataba. Fedha iliyoshikiliwa itatolewa katika kipindi kitakachokuwa kimeonyeshwa kwenye Masharti Maalumu ya Mkataba Fedha anayotakiwa kulipwa Mtoa Huduma chini ya Ankara yoyote ile italipwa na Mwajiri kwenda kwa Mtoa Huduma katika kipindi kitakachokuwa kimetajwa katika Masharti Maalumu ya Mkataba baada ya Ankara kuwasilishwa na Mtoa huduma. 21.3 Malipo ya Mwisho Ankara ya mwisho italipwa katika siku 28 za kazi baada ya tarehe ya kuwasilishwa kwa Mteja ilimradi huduma zote, masahihisho na matengenezo, kama yapo yatakuwa yametekelezwa katika kiwango kitakachomridhisha Mteja.21.4 Ucheleweshwaji wa Malipo‌‌ Kama Mteja atashindwa kufanya malipo katika muda uliotajwa, Mteja atamlipa Mtoa Huduma riba katika kiwango kilichotajwa kwenye Masharti Maalumu ya Mkataba.21.5 Makato ya Malipo Mteja atakuwa na haki ya kukata fedha kiasi cho chote, fedha ya malipo ya awali au madeni yanayolipika kutoka kwa Mtoa Huduma kwenda kwa Mteja kutokana na fedha yoyote anayoweza kulipwa Mtoa Huduma na Mteja chini ya mkataba huu ilimradi kifungu hiki hakitaathiri marekebisho yoyote kwa amri ya sheria pengine ambayo mteja anaweza kuwa na haki ya kurudishiwa fedha yoyote kama hiyo. 21.6 Malipo kwa Wafanyakazi Kama kutatokea kushindwa kulipa mishahara/ujira na fidia nyingine zinazopaswa kulipwa wafanyakazi na /au malipo ya kukodisha zana/magari na vifaa chini ya mkataba huu, mteja atakuwa na haki ya kushikilia malipo ya Mtoa Huduma. Mteja atatumia fedha alizoshikilia kuwalipa wafanyakazi wa Mtoa Huduma mishahara yao na fidia nyingine na madeni ya kukodisha vifaa. Malipo kama hayo yatachukuliwa kuwa ni malipo yaliyopokelewa na Mtoa Huduma kutoka kwa Mteja chini ya mkataba huu. Kifungu 22:Malipo ya Ucheleweshaji Huduma Kama Mtoa Huduma atashindwa kutoa huduma katika muda uliotajwa kwenye mkataba au katika muda wowote wa nyongeza ulioruhusiwa na Mwajiri, Mtoa...