KUSULUHISHA MIGOGORO NA KUVUNJA MKATABA‌ Zitsanzo za Migwirizano

KUSULUHISHA MIGOGORO NA KUVUNJA MKATABA‌. Kifungu 23: Kusuluhisha Migogoro 23.1 Kama migogoro ikitokea itasuluhishwa kwa majadiliano ya pande zote. Kama baada ya siku thelathini (30) pande hizo zimeshindwa kumaliza mgogoro au tofauti zao kwa majadiliano ya pamoja, upande wowote ule utawasilisha mgogoro huo kwa maandishi kwa Mwamuzi na kutoa nakala kwa upande mwingine. 23.2 Mwamuzi aliyetajwa katika Masharti Maalumu ya Makataba atatoa maamuzi kwa maandishi katika muda wa siku ishirini na nane (28) baada ya kupokea taarifa ya mgogoro. 23.3 Mwamuzi atalipwa kwa saa kwa kiwango kilichotajwa kwenye Masharti Maalumu ya Mkataba pamoja na kurudishiwa gharama za aina ya matumizi kama yalivyobainishwa katika Masharti Maalumu ya Mkataba na gharama hiyo itagawanywa kati ya Mteja na Mtoa Huduma kwa uamuzi wowote utakaofikiwa na Mwamuzi. Upande wowote unaweza kupeleka uamuzi wa Mwamuzi kwa Msuluhishi kwa maandishi katika kipindi cha siku ishirini na nane (28) baada ya uamuzi ya Mwamuzi. Kama hakuna upande wowote utakaokuwa umepeleka mgogoro kwa Msuluhishi katika muda wa siku ishirini na nane (28) zilizotajwa hapo juu, uamuzi wa Mwamuzi utakuwa ndiyo wa mwisho na itabidi ufuatwe. 23.4 Kama Mwamuzi atajiuzulu au kufariki au kama Mteja na Mtoa Huduma wakikubaliana kuwa Mwamuzi hafanyi kazi yake ipasavyo kulingana na vifungu vya Mkataba, Mwamuzi mpya atateuliwa kwa pamoja kati ya Mteja na Mtoa Huduma. Kama kuna kutokubaliana kati ya Mwajiri na Mtoa Huduma katika muda wa siku 30, Mwamuzi atateuliwa na Mamlaka ya kuteua itakayotajwa katika Masharti Maalumu ya Mkataba kwa maombi ya upande wowote katika muda wa siku kumi na nne(14) tangu kupokelewa kwa ombi hilo. 23.5 Mgogoro au tofauti yoyote ambapo notisi ya kusudio la kuanza usuluhishi imetolewa kulingana na kifungu hiki itamalizwa kwa usuluhishi. Usuluhishi unaweza kuanza kabla au baada ya kuanza kutoa huduma chini ya mkataba.23.6 Usuluhishi utaendeshwa kulingana na taratibu za usuluhishi kama zilivyochapishwa na taasisi iliyotajwa na mahali palipoonyeshwa katika Masharti Maalumu ya Mkataba.‌ 23.7 Bila kujali uwepo kwa usuluhishi wa aina yoyote, (a) Pande zote zitaendelea kutekeleza majukumu yao chini ya mkataba isipokuwa kama wakikubaliana vinginevyo; na (b) Mwajiri atamlipa Mtoa Huduma fedha yoyote Mtoa Huduma anayodai.Kifungu 24: Uvunjaji wa Mkataba 24.1 Kama Mtoa Huduma anashindwa kuanza kutoa huduma katika muda uliopangwa au kuna sababu za kutosha kuamini kuwa hatakamilisha huduma katika muda uliopangwa au kuna ucheleweshaji uliokiuka tarehe ya kukamilisha au ...